MC ON THE MOVE... BOOK HIM 0712226808

MC ON THE MOVE... BOOK HIM 0712226808
FOR YOUR WEDDING, SENDOFF, CRUSADE FUND RISING EVENT.CALL 07132268

Sunday, September 16, 2012

WANAWAKE WA CITY HARVEST WAVUNJA UKIMYA

Wanawake wa Kanisa linalokua kwa kasi la CITY HARVEST ambalo ni mahususi kwa Wanataaluma vijana na wanafunzi wa Vyuo wameendesha ibada leo kanisani hapo na kuacha historia kubwa.. akihubiri katika ibada hiyo Mama Askofu Masawe amesema wanawake ni watu wa muhimu sana katika jamii kwani hata wafalme walipokuwa na matatizo walikuwa wakiwauliza wanawake.

Pia amesema hata Yesu alifutwa miguu yake kwa nywele za mwanamke pia siku anafufuka alionwa kwanza na wanawake.. hata hivyo akiendelea kuhubiri alisema wanawake wanatakiwa kuwa watiifu kwa waume zao kwani ndivyo walivyoagizwa na Mungu,

Wakati akiendelea kuhubiri akagusia kitu kimoja ambacho ni muhimu sana kwa kanisa kwamba Kanisa likiwa na wanawake waliojitoa kwa huduma linaweza kufika mbali na kuwa na Nguvu ya Mungu kwani wanawake wakiomba Mungu anajibu maombi,

Baadaye Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Yared Dondo akihitimisha ibada hiyo iliyokuwa imejaa Nguvu ya Mungu tangu wakati wa ibada ya kusifu na kuabudi hasa wakati Mwimbaji wa kikundi cha kusifu na kuabudu Upendo Chavala alipoimba wimbo wa HE HAS GIVEN ME VICTORY ambapo wazee wa kanisa na wachungaji waliishiwa na uzalendo na kujikuta wote wamejaa mbele na kucheza, Pastor Dondo alisema tangu kanisa hili lilipoanza pale ndani ya Mlimani City wanawake wa City Harvest walikuwa wakiomba kila siku ya Jumamosi pale Church Ofice Mwenge na anachokiona sasa anaamini ni matokeo ya maombi yale.

Wanawake wa City Harvest walimpatia zawadi mama askofu pamoja na kutoa zawadi kwa kanisa ambayo kwa niaba yake walimkabidhi mchungaji kiongozi Yared Dondo.

habari hii imeandaliwa na the blogger Lawrence Mwantimwa..

TUPATE HABARI ZAIDI KATIKA PICHA..

PASTOR BETHA KIPILIMBA AKIMKABIDHI ZWADI MHUBIRI MRS. ASKOFU MASAWE


SIFA IKAZIDI KUCHANGANYA WEE.. IKAWA HOT ZAIDI


HAYA MBUNGE TO BE





MHUBIRI AKAKAMATA MADHABAHU

WANAWAKE WA CITY HARVEST WAKAOMBEWA MA MAMA ASKOFU

UPENDO CHAVALA BINTI WA YESU AKASIMAMA NA KUSOMA POEM I
LIYOWAGUSA WATU WENGI SANA NA ALIISOMA KWA
USTADI WA HALI YA JUU MNO...





PATOR DONDO AKIKABIDHIWA ZAWADI TOKA KWA AKINA MAMA


SIFA IKACHANGANYA WATU GAFLA WAKAJAA MBELE






HAPA WANA MUSIC GEBO, JONAS NA TITO WAKIWA SUPPORT
 WAKINA MAMA 


PRAISE TEAM WAKIJIACHIA MBELE ZA BWANA

THE BLOGGER LAWRENCE MWANTIMWA NA ANDE
WAKIJIHUSISHA IN GOD'S PRESENCE

MEZA KUU TOKA KULIA NI PASTOR KIPILIMBA, BERTHA, MRS BISHOP MASAWE
PASTOR MATILDA, YARED, MAGDALENA NA PASTOR PROF. RWEBANGIRA


HAPA SIJUI HATA ILIKUWAJE ?

THE BLOGGER NAYE HUYOO MBELE AKIJICHANGANYA NA
WAPENDWA WENGINE






PPAISE TEAM YA WANAWAKE WOTE WA KANISA
IKASIMAMA KUIMBA TENZI


No comments:

Post a Comment