Mji wa ZANZIBAR hivi karibuni uligubikwa na vurugu mpya za kupinga muungano na kuwalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa kikundi cha uamsho waliokuwa wakiandamana,
tukuio hilo lilitokea katika eneo la mahonda mkoa wa kaskazini unguja ambapo wafuasi hao walikuwa wakiandamana kuelekea katika mhadhara uliopangwa kufanyika katika eneo la Donge nje kidogo ya mji wa Unguja,
hivi ni kweli njia pekee za kupinga muungano ni kufanya fujo? nafikiri kuna njia nyingi za kuwasilisha hoja nzuri na nzito zitakazowafanya watawala kukaa mezani na kujadili upya misingi na makubaliano yaliyofanywa na viongozi wetu tunaowaenzi mpaka leo siku hizo, kufanya fujo na maandamano ni kuhatarisha maisha ya watoto na akina mama ambao ni waathirika wakubwa wa fujo na machafuko kwani uwezo wao wa kukimbia na kujisaidia wakati wa hizo movements ni mdogo sana, kwa hiyo ushauri wa bure kwa hao wanauamsho no kutumia njia mbadala kwani mtu anaetumia nguvu mara nyinngi ni yule aliyeshindwa kwa hoja kwa hiyo basi nashauri hoja zitumike zaidi ya nguvu.
wanasiasa kama Raisi wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein hivi karibuni alisema wote wanaopinga na kuukataa muungano hasa wazanzibari wasubiri Tume ya katiba ifanye kazi yao na wao watoe maoni huko kuliko kutumia fujo na nguvu bila matiki.
facebook