Kama kuna vitu vinanipa uhakika wa mimi kuja kuwa Raisi wa Nchi hii ni ile kitu inaitwa Strong Determination inayo tekenya na kuusumbua moyo wangu kila siku.. huwa nakumbuka miaka kadhaa iliyopita kabla sijaanza Shule kwa mara ya pili baada ya kuacha shule nikiwa form two mwaka 1994 huko mkoani Mbeya, nilikuwa ninajihusisha na biashara za Umachinga na mazao kama KARANGA NA ULEZI nikivitoa Nchini Zambia na kuleta Tanzania, wakati huo nakumbuka watu kama STEPHEN MWAISUMO NA FIKIRI, BILA KUMSAHAU BENJAMINI MWALUSAMBA ambao tulikua tunasafiri wote kwenda Zambia.
SIKU NAAPISHWA KUWA RAISI WA TUMAINI UNIVERSITY DAR ES SALAAM COLLEGE |
Kitu cha ajabu ni kwamba wakati wote huo nilikuwa najutia sana maamuzi yangu ya kuacha shule kwani nilikua najua kama ningesoma ningekuwa President wa Nchi hii sasa ndo hivyo tena nilikua nimeacha shule.. mawazo na mateso ya moyoni yaliendelea kunitesa mpaka siku moja nilipoamua kurudi Shule tena nikiwa na Miaka 21 na nkaamua kuanza kidato cha kwanza kabisaa......
NIKIWA KWA KIKAO CHA MARAISI WA VYUO VIKUU KUJADILI MASUALA YA BODI YA MIKOPO UKUMBI WA DAR ES SALAAM INTERNATIONAL CONFERENCE CENTRE |
nikiwa natamani sana kutokusomea mkoni mbeya ndipo nilipoamua kuhamia Jijini ar es salaam ambapo nilianza kidacho cha kwanza shule ya Kijitonyama na baadaye kuhamia Air Wing secondary, kisha A Level Lyamungo Kilimanjaro na kisha kuhamia MBEYA HIGH SCHOOL nilipomaliza kidato cha sita.. na baadaye kujiunga na CHUO KIKUU CHA TUMAINI DSM...
nakumbuka Mungu aliniwezesha kunipatia marafiki wengi sana akiwemo Godwin Gondwe, Paul Mngngo, James Mwangamba, Robert Raphael, Emmanuel Seme, Joseph Msami, Ndganza Mzonya, Shadrack Mkama, Isaac Gamba, Haris Kapiga, Ambele Chapa Nyota, Fredy Kameta na wengine wengi sana ambao walikua wakinitia Moyo sana wakati wote wa kusoma kwangu..
GONDWE NDIO RAFIKI ALIYENISHAURI NISOME TUMAINI UNIVERSITY.. HAPA AKIFURAHI NAMI SIKU YA GRADUATION YANGU |
Sasa kilichinivutia sana ni hiki hapa..... Ndoto yangy na safari yangu ya SIASA NA Kupenda kuwa Raisi ikaanza kustawi kwa kasi kubwa sana... nilikwa O Level nakumbuka nilishinda nafasi ya HEAD PREFECT kwa asilimia zaidi ya 90 TOFAUTI NA mpinzani wanu, nikiwa CHUO KIKUU PIA niliwashinda wapinzani wangu wawil na kuweka HISTORIA YA KUWA RAISI WA KWANZA KUGOMBEA NA KUWASHINDA Wagombea wa LLB chuoni kwangu ambao ndo walikuwa wakigombea na kushinda kila mwaka..
Nilpokuwa RAISI wa Chuo pia nilijiandaa kugombea nafasi RAISI WA MARAISI WA VYUO VIKUU na badaye Rafiki yangu kipenzi NOEL KATONGO akaniomba nimuachie agombee hasa baada ya kuona mguso niliokuwa nao kwa maraisi wengine... lakini sikuishia hapo nikapata nafasi ya kuwa COMMISSIONER wa TAHLISO NA KUONGOZA MIKA YA DSM, MOROGORO, TANGA, LINDI NA MTWARA..
kwa upande wa huduma za kiroho pia niliweza kuwa RAISI WA CASFETA TANZANIA kwa miaka miwili mfululizo, makamu wa raisi kwa mwaka mmoja na Katibu mkuu kwa mwaka mmoja
na kwa sasa ni Chair man wa vijana wa City Harvest... na Rais wa CASFETA ASSOCIATES Tanzania...
NIKIMALIZA KUENDESHA SHUGHURI YA MH. WILLIAM LUKUVI WAZIRI. |
AFTER SERVICE NA MH. MBUNGE NAOMI KAIHULA..(CITY HARVEST) |
MBEYA HIGH SCHOOL.. KIDATO CAH SITA MWAKA 2007.. NIKITAFAKARI MAISHA YANGU CHUO KIKUU YATAKUWAJE? |
NIKITOA SPEECH BAADA YA KUCHANGISHA PESA ZA KUWASOMESHA WANAFUNZI WANAOTOKA KTK FAMILIA ZISIZO NA KIPATO.. CCC |
No comments:
Post a Comment