MC ON THE MOVE... BOOK HIM 0712226808

MC ON THE MOVE... BOOK HIM 0712226808
FOR YOUR WEDDING, SENDOFF, CRUSADE FUND RISING EVENT.CALL 07132268

Thursday, June 20, 2013

KAMETA KUZINDUA ALBAM YA OMBA LOLOTE DAR... Call 0713 226808 au 0767226808

FRED KAMETA (MUIMBAJI NA PRODUCER MAARUFU NCHINI)

FRED... 0656111118 NA 0755755223

Muimbaji wa Nyimbo Za Injili Tanzania na Duniani Pote na mtengeneza Ala za Music Nchini Maarufu kwa Jina ka FRED KAMETA ameamua Kuvunja Ukimya na Kuamua kuzindua Albam yake inayowika kwa jina la OMBA LOLOTE, Akiongea na Meneja wake LAWRENCE MWANTIMWA Fred Kameta amesema kwamba amepata msukumo wa Ndani wa kuingia kwa miguu yote miwili katika huduma hii ya kumtumikia Mungu kwa njia ya Uimbaji, Fred amesema kwamba amekuwa muimbaji kanisani na kwenye mikutano ya Injili Tanzania pamoja na kwenye Matamasha mbalimbali ya Uzinduzi na mengineyo lakini hakuwa ameamua kuwekeza katika huduma hii lakini kwa sasa ameamua kufanya hivyo....


Kameta amesema amekuwa akiwatengenezea Ala za Music pamoja na Kurecod nyimbo za waimbaji wengi sana wa Music Tanzania kama vile Abihudi Misholi, Jojo Jose, Ambele Chapa Nyota, David Robert, Stela Swai na wengine wengi ikiwa ni pamoja na Agape Super Power Praise Team...
Fred Pichani amesema kwamba anatamani kuona watu wengi zaidi wakiguswa na uimbaji wake wenye mguso wa Roho mtakatifu...


Akiongea hivi karibuni Meneja wa Fred Kameta Ndugu Lawrence Mwantimwa amesema kuwa katika Tamasha hilo kutakuwepo na waimbaji wengi sana kumsindikiza rafiki yao Fred Kameta wengi wao wakiwa ni wale waliowahi guswa na huduma ya Producer huyu maarufu katika nyanja ya kutengeneza Music, na amesema kwamba pamoja na hao pia kutakuwepo na waimbaji kutoka Uganda na Kenya watakao kuja kumpa suport Fred, akiwataja baadhi ya waimbaji

Lawrence amesema ni pamoja na Mellody Ndichu toka Kenya, Price George toka Uganda, kwa Tanzania ni David Robert, Ambwene Mwasongwe, Rungu la Yesu, Joseph Nyuki. Joshua Makondeko, Stella SWAI, Happy Kamili, Jojo Jose na ACAPELA Singers...


Tamasha limepangwa kufanyika tarehe 14 July 2013 katika ukumbi wa Sinza Christian Center Sinza Kumekucha Dar es Salaam Tanzania....kuanzia saa Nane mchana na kuendelea....

WAFUATAO NI WAIMBAJI MAARUFU WATAKAO KUWEPO KUMSINDIKIZA FRED KATIKA UZINDUZI WAKE

PRICE GEORGE KUTOKA UGANDA NAYE ATAKUWEPO KUMSINDIKIZA FRED


RUNGU LA YESU MZEE WA GOSPEL HIP HOP ATAKUWEPO


JOSHUA MAKONDEKO MZEE WA MALIPO NDANI YA NYUMBA


MUNGU AKUPE NINI? MUIMBAJI WA KIMATAIFA MELLODY NDICHU TOKA KENYA ATAKUWEPO


KIFAA CHA YESU JOSEPH NYUKI ATAMALIZA KAZI KWA SEBENE ZA UKWELI


USIKOSE NA MTAARIFU NA RAFIKI YAKO.... WOTE MNAKARIBISHWA